Diamond Platnumz — Mbagala

Diamond Platnumz Mbagala

Текст песни

Busara na upole

Na hekima nilorithi kutoka kwa mama yangu, mama

Vyote haukuvijali

Ukaona silingani kabisa kuwa na wewe

Ka kuti na mkole

Ukakata kabisa na shina la penzi langu nana

Eti kisa mali

Ukaona bora uniache mimi na uolewe

 

Ile siku shekhe namuona anachoma ubani

Unavishwa pete unakuwa mke wa fulani

Nliumia sana, sana

Ile siku shekhe namuona anachoma ubani

Unavishwa pete unakua mke wa fulani

Niliumia sana, niliumia sana, sana

 

Tatizo kwetu Mbagala

Hapa nyumba mbele jalala

Tatizo kwetu Mbagala

Ukaona mapenzi siwezi

 

Ungejua jinsi gani

Machozi nlolia kwa uchungu wa penzi langu na

Mwenzio jinsi gani

Vile nimeumia moyoni

Hata kupendwa sitamani

Utamu wa mapenzi mwenzako umekula kwangu ma

Mwenzio sitamaani

Hata raha tena mi sioni

 

Ah naskia hivi sasa una mtoto anaitwa Mamu

Vile akinuna mpaka atabasamu

Mmefanana sana, sana

Mi mwenzako tena mapenzi mi sina hamu

Tena na mpango wa kuhama Dar Es Salaam

Nataka niende mbali

Niepuke vita na walimwengu mi mwenzenu siwezi

 

Tatizo kwetu Mbagala

Hapa nyumba mbele jalala

Tatizo kwetu Mbagala

Ukaona mapenzi siwezi

 

Nasema Mbagala, Mbagala, Mbagala aa aaha

Mbagala, ukaona mapenzi siwezi

Nasema Mbagala (Mbagala), Mbagala (Mbagala)

Mbagala (Mbagala) ee eh

Mbagala, ukaona mapenzi siwezi

 

Tatizo kwetu Mbagala

Hapa nyumba mbele jalala

Tatizo kwetu Mbagala

Ukaona mapenzi siwezi

 

Клип «Mbagala»

Видеоролики хранятся и модерируются сервисом YouTube. Отказ от ответственности

Заказать перевод Прислать свой вариант перевода

Текст песни Diamond Platnumz Mbagala предоставлен в ознакомительных целях для личного развития.