Diamond Platnumz — Lala Salama

Diamond Platnumz Lala Salama

Текст песни

Lala salama

Matatizo, chuki, lawama

Ukilala lala salama, kumbatia picha yangu

Na kama ukinikumbuka sana nipigie simu yangu

Uki-ukilala lala salama, kumbatia picha yangu

Matatizo, chuki, lawama vumilia mpenzi wangu

Najua wivu ndo mapenzi, ila chunga usizidi

Si unajua kwako sijiwezi, ila dhiki mmebidi

Mi nilitamani sana mi kuwa nawe

Tuwe wote usiku na mchana

Kilichonifanya mi nipagawe

Sina chochote cha kuwalisha wana

Niliupokea kwa unyonge msiba wa kaka Bonda

Ile barua yako ya mwisho ilinitonesha vidonda

Usije nilali kipenzi changu

Ukadhani nimekumbwa na pepo la starehe

Mambo bado magumu kwangu

Afadhali hata ya jana, ya kesho niombee

Ukilala lala salama, kumbatia picha yangu

Na kama ukinikumbuka sana nipigie simu yangu

Uki-ukilala lala salama, kumbatia picha yangu

Matatizo, chuki, lawama vumilia mpenzi wangu

Ile “kua uone”, nilidhani maghorofa

Ah aa kumbe mwana ukome, hakuna cha kuokota

Mi bado nakaza moyo changu kipenzi

Ila naumia kwa kuwa mwenyewe

Natamani ila siwezi, nazitafuta nije kula na wewe

Msalimu mama nyumbani, usiseme kama nahenya

Tai, mfiche mpe imani, karibu ntakuoa chema

Usije nilali kipenzi changu

Ukadhani nimekumbwa na pepo la starehe

Mambo bado magumu kwangu

Afadhali hata ya jana, ya kesho niombee

Ukilala lala salama, kumbatia picha yangu

Na kama ukinikumbuka sana nipigie simu yangu

Uki-ukilala lala salama, kumbatia picha yangu

Matatizo, chuki, lawama vumilia mpenzi wangu

Клип «Lala Salama»

Видеоролики хранятся и модерируются сервисом YouTube. Отказ от ответственности

Заказать перевод Прислать свой вариант перевода

Текст песни Diamond Platnumz Lala Salama предоставлен в ознакомительных целях для личного развития.