Тексты и переводы песен

Kosa Langu

Ah! Barua yako uliyotuma kwa Ricardo Momo nimeisoma
Ila nimechelewa kuijibu sababu moyoni imenchoma
Eeh, nliyo yategemea tofauti na nlicho kiona
Hata naandika hii barua huku roho yangu inansonona
 
Umesema nichane nguo pia funguo
Umeirudisha sawa
Simu niziweke kituo na sio chaguo
Nikome kabisa sawa
Umesema hata ile picha nzuri
Nliyo kukumbatia niichane sawa
Ila kinachoniumiza
Mbona moja umesahau
 
Kosa Langu Kosa Langu
Hujaniambia
Na kuniacha peke yangu
Ukanikimbia
Ila mbona kosa langu
Hujaniambia
Nami nikabiki peke yangu
Ukanikimbia
 
Aah!
Mbona ukanichimbia kaburi ningari bado mzima
Niife nizikwe vizuri nipotee kabisa kimya
Licha ya matendo mazuri kwa upendo na heshima
Moto ukachochea tanuri ukachoma wangu mtimaa
 
Natamani hata ningepata nafasi
Muda wakati kukutazama
Unione hata japo sura
Unitazame macho yangu
Mwenzako wimbi limenipiga kasi
Langu jahazi limezama
Mnyonge mwana Sanura
Wee ndio ulikuwa furaha yangu
 
Tatizo hata nkilia wa kunifuta machozi sina
Sawa na gari lisio na gear
La kuiforce ipande mlima
Ndio maana siishi kulalama
Japo jibu moja tuu
Linaloniumiza
Mwenzio bado sijaelewa
 
Kosa Langu Kosa Langu (Kosa Langu)
Hujaniambia (Hujaniambia)
Na kuniacha peke yangu (Peke yangu)
Ukanikimbia (Ukaenda)
Ila mbona Kosa Langu (Kosa Langu)
Hujaniambia (Hujaniambia Bado)
Nami nikabi peke yangu (Peke yangu)
Ukanikimbia (Ukaenda Ooh!)
 
(Oh moyo!)
Moyo wangu umevunjika una magongo
(Oh moyo!)
Kila sehemu nayoshika kinyamazongo
(Oh moyo!)
Hata chozi likifutika linabaki tongo
(Oh moyo!)
Najitahidi kulidhika ila nna kinyongo
 
(Oh moyo!)
Moyo wangu umevunjika unaa jamani
(Oh moyo!)
Hhhhmm hmm
 

Понравилась песня? Будем очень благодарны, если вы расскажете о ней друзьям:



Послушать песню и посмотреть клип "Kosa Langu"

Видеоклипы к песне подбираются автоматически сайтом youtube.com. Отказ от ответственности

Текст песни Diamond Platnumz Kosa Langu предоставлен в ознакомительных целях для личного развития.