Тексты и переводы песен

Iyena

Hmm, ah leo chereko chereko mwanenu nimekuwa
Zile kuringa mideko itapungua
Asante mama, ulinifunza nkajua
Baba kasema kuomba mwiko raha ya chumvi kununua
Tena si kwa nazi si hirizi za waganga
Kwa baraka za baba na mama tu na dua
Waambie paparazi, pingamizi wenye viranga
Waliosema hayawi hayawi yamekuwa
Ooooh oh!
 
Iyena Iyena
Iyena Iyena
Iyena Iyena
Kwaheri tutaonana
Iyena Iyena (aai ooh)
Iyena Iyena (aai Iyeena)
Iyena Iyena
Ntawakumbuka sana
 
Oooh ndoa baraka ukipata ushukuru
Maana wanayoililia ni wengi sana
Kwetu talaka kuitoa ni kufuru
Nimefunzwa vumilia, niushinde ujana
Ili kesho mahususi kusudi wasinong'one
Embu nichumu niringe washushuke
Na hii pete ya harusi nakuvisha waone
Wakale sumu wavimbe wapasuke
 
[Diamond Platnumz & Rayvanny]
Eeh!
Ati nashika nanga nteke nsichomoke ndani
(Anameremeta)
Futa namba wablock vimada wa zamani
(Anameremeta)
Sio vijembe vya kanga waziwazi mambo hadharani
(Anameremeta)
Waliopanga mwenye nyumba kaja ndani
(Anameremeta)
 
Iyena Iyena (aah iyoyo)
Iyena Iyena (aah eeeh)
Iyena Iyena
Kwaheri tutaonana (oh, kwaheri Baba, Mama)
Iyena Iyena (Iyeeena)
Iyena Iyena (aah eeh)
Iyena Iyena
Ntawakumbuka sana
 
[Rayvanny]
Imefika tamati tulisubiri kitambo
Leo samaki kanasa kwenye chambo
Pongezi kwa kamati yanavutia mapambo
Napata picha safi litanikoma bundle
Mwanamke usafi gaga kulisugua
Mume akirudi sharti viatu kumvua
Kitandani marashi massage kumchua
Kisha anza sayansi, viuno kutengua
Mambo ya kuzima taa si mahaba ni kuwanga
Washa japo ka mshumaa mumeo aone shanga
 
[Rayvanny]
Eeeh!
Makeup kinanda kaka suit kama mbunge
(Anameremeta)
Mulo changa muda kujipooza na punje
(Anameremeta)
Momo ndani, Shivo amekuja na Fumbwe
(Anameremeta)
Kula chanda ukishiba ruksa kafunge
(Anameremeta)
 
Iyena Iyena (aah iyeee)
Iyena Iyena (aah iyoyo)
Iyena Iyena
Kwaheri tutaonana (eh, kwaheri Baba, Mama)
Iyena Iyena (Iyeee)
Iyena Iyena (hmm)
Iyena Iyena
Ntawakumbuka sana
 
[Diamond Platnumz & Rayvanny]
Saa nataka kusasambua (sasambu)
Me nasasambua (sasambu)
Abidadi nasasambua mimi (sasambu)
Sasambua tuone
Mguu moja juu (sasambu)
Usishushe chini (sasambu)
Cheza jitazame (sasambu)
Sasambua tuone
 
Aisha Kimobitel (sasambu)
Nipe za Balotelli (sasambu)
Nyonga kibaiskeli (sasambu)
Sasambua tuone
Akaa kama unashika ukuta (sasambu)
Ifanye unashusha (sasambu)
Taratibu zungusha (sasambu)
Sasambua tuone
 
Sasambu, sasambu, sasambu
Sasambua tuone
Kama unawasha bajaji (sasambu)
Imwagie na maji (sasambu)
Tuwakomeshe vizazi (sasambu)
Sasambua tuone!
 

Понравилась песня? Будем очень благодарны, если вы расскажете о ней друзьям:



Послушать песню и посмотреть клип "Iyena"

Видеоклипы к песне подбираются автоматически сайтом youtube.com. Отказ от ответственности

Текст песни Diamond Platnumz Iyena предоставлен в ознакомительных целях для личного развития.