Haunisumbui
(Ayolizer)
Si kokoko si kandambili
Yaani vyote havikupendezi
Mwana ngoko usonawili
Tope bin uterezi
Utaishia kututabiri
Tubomoke inasonga miezi
Mola ameshatakabiri
Usijichoshe halivunjiki penzi
Ona! umekosa nuru
Umekosa bahati huna
Unaitwa kunguru
Ukifika wananuna
Ndo ndo ndo mwana chururu
Asiye mbuzi wataka chuna
Mengine nisikufuru, mmmh
Hazikukai maskara
Wala make up zinakushuka
Uso umekuparara
Mwili shock up, zimetenguka
Uso sauti ya stara
Kwa kudeka unawehuka
Jibwa koko la Mbagala
Unabweka na kubwetuka wala!
Wala haunisumbui wala
Wala haunisumbui wala
Wala haunisumbui wala
Wala haunisumbui wala
Na hizo post mara kubebana
Mara eti mnabusu mtamaliza bando
Unaowatuma kunitukana
Siogopi mashushu me wala michambo
Kutwa kwa mapage feki
Kama lokole linahusu...?
Mkwe akutaki eti
Mwenzangu pole mbona kuntu
Vimeseji kujitumisha
Kwa ndugu zangu marufuku
Nyota imekufubika
Usifosi umaarufu
Upepo wa kisulisuli
Unakuchukuwa na nuksali
Tanga lipulipuli
Wanakununua kwa mizani
Kwangu mpambe shughuli
Najiashua burudani
Na toto nzuri nzuri
Nimelitua tuli ndani ii
Ona umekosa nuru
Umekosa bahati huna
Unaitwa kunguru
Ukifika wananuna
Ndo ndo ndo mwana chururu
Asiye mbuzi wataka chuna
Mengine nisikufuru
Usiye wa shaba wala chuma
Wala haunisumbui wala
(Wala hamunikondeshi)
Wala haunisumbui wala
(Mujipost mainstagram)
Wala haunisumbui wala
(Wala hamunitetereshi)
Wala haunisumbui wala
(Waaalah)
(Wasafi)