Diamond Platnumz — Binadam

Diamond Platnumz Binadam

Текст песни

Eyoh…

Yoh I'm back Bob Junior, I'm back

Acha vita ianze

Wamechelewa

 

Ni we pekee unaejua wangapi binadamu wabaya (wabaya)

Ndugu, rafiki, nani ana roho safi

Nani ana roho mbaya (mbaya)

Ni we pekee unaejua wangapi binadamu wabaya

Mola, naomba nilinde niwe na upendo wa dhati

Wote niishi nao sawa

 

Nilipouanza mziki, mbali na dhiki

Nimekutana na matatizo sana

Sikuwa rafiki, sithaminiki

Bado kidogo mie tu nikate tamaa

Wangu moyo

Ulivumilia dharau na masimango mi

Mi wangu moyo

Ulivumilia utumwa na manyanyaso di

 

Yaani nahangaika usiku kucha naambulia patupu

Nilikuwa naumia

Moyoni najipa moyo kesho ntakuwa maarufu

Mwisho wa siku nafulia

Ile nahangaika usiku kucha naambulia patupu

Nilikuwa naumia

Najipa moyo kesho ntakuwa maarufu

Mwisho wa siku nafulia

 

Ni we pekee unaejua wangapi binadamu wabaya (wabaya)

Ndugu, rafiki, nani ana roho safi

Nani ana roho mbaya (mbaya)

Ni we pekee unaejua wangapi binadamu wabaya

Mola, naomba nilinde niwe na upendo wa dhati

Wote niishi nao sawa

 

Kidogo nakula na mama yangu

Siwezi kuwasahau na ndugu zangu

Upendo popote alipo kwa baba yangu

Japo alinikataa

Aa bata nakulaga mi na rafiki zangu

Tunacheza Reggae na masikini wenzangu

Alazwe pepa peponi na bibi yangu

Mjukuu wake Sanana

 

Sababu ya ugumu wa maisha

Na maumivu ya mapenzi nikaandika "Kamwambie"

Ndo hapo hustle zikaisha, kabariki Mwenyezi watanzinia wanizimie

Asa hivi kwenye tamasha tu likitajwa jina watu wanashangilia

Wengine furaha inazidi kina hadi kabisa wanalia

Asa hivi kwenye tamasha yaani ikitajwa jina watu wanashangilia

Wengine furaha inazidi kina hadi kabisa wanalia

 

Ni we pekee unaejua wangapi binadamu wabaya (wabaya)

Ndugu, rafiki, nani ana roho safi

Nani ana roho mbaya (mbaya)

Ni we pekee unaejua wangapi binadamu wabaya

Mola, naomba nilinde niwe na upendo wa dhati

Wote niishi nao sawa

 

Eii tena wabaya sana

Ouu wanakatisha tamaa

Eii uh wabaya

Tena wabaya

Ouu aah

Sana, wabaya sana

Wabaya sana

Mmh wabaya sana

 

Клип «Binadam»

Видеоролики хранятся и модерируются сервисом YouTube. Отказ от ответственности

Заказать перевод Прислать свой вариант перевода

Текст песни Diamond Platnumz Binadam предоставлен в ознакомительных целях для личного развития.