Acha Nikae Kimya
Mama ananambia Naseeb
Mi ni mtu mzma nawe ndo nakutegemea
Yanayotokea jaribu kupiga kimya usidiriki ata kuongea
Mara nasikia vya aibu Konda, Gwajima eti ugomvi umekolea
Kuchunguza karibu ni binti mmoja kwa mitandao wanachochea
Najaribu kunyamaza, ila moyo hautakii
Unanambia eti Simba japo unguruma uisemee hakii
Ooh najaribu kunyamaza ata Laizer ataki yoo
Anasema walau nena kidogo (hiih!)
Na mashabiki Dangote
Wananambia mbona husemi chochote, ah
Si uko nao siku zote
Ama ulezi unafanya uogope, ah
Na media pande zote
Wanalalama kiongozi atoke eh
Nchi inaingia matope
Niende wapi na mi mtoto wa wote
Yaani lawama...
Wacha nikae kimya
Mmh nisiongee (kimya)
Ooh ninyamaze mimi (nikae kimya)
Nisiseme (kimya)
Mama kanambia (wacha nikae kimya)
Ooh nifunge mudomo (kimya)
Mie bado mdogo sana (nikae kimya)
Nisiseme (kimya)
Mmh ni mengi majaribu
Najatahidi epuka yasije nicost
Japo mengine swadakta mengine hayana maana
Rafiki kipenzi wa karibu
Hata nyimbo yake sikuweza ipost
Ila alivokamatwa iliniumiza sana
Mitandaondi kila kona
Uongo na ukweli unashonwa
Kila nyumba inanong’ona
Ah oh Tanzania
Mara kimbembe Dodoma
Bunge upinzani wamegoma
Juzi akapotea na Roma
Ohh Tanzania, ooh
Najaribu kunyamaza, Makame hataki yooh
Ananambia walau nena kidogo
Nyumbani nafungua gate
Niende kwa Mangi nunua super gate eh
Napewa za chini ya kapeti
Kuna redio imevamiwa kefti eh
Napita kwenye (magazeti)
Nakuta rundo la watu (wameketi)
Eh, badala ya kutafuta cent
Wanabishana tu mambo ya vyeti
Wacha nikae kimya
Ooh nisiongee (kimya)
Ninyamaze kabisa (nikae kimya)
Eh ulimi koma (kimya)
Usije kunipoonza! (acha nikae kimya)
Nifunge bakulu lanhu! (kimya)
Nikojoe nikalale (nikae kimya)
Mi bado mdogo sana (kimya)
Mama kanambia
Oh najiuliza (waaaapi)
Najiulii (waapi)
Tunakwenda wapi (waapi)
Kila siku maneno (waaaa)
Ah tuacheni jamani (waaapi)
Mi na we ni taifa moja (waaapi)
Kambarage baba mmoja (waaaa)
Sa tofauti za nini tushikamane
Tukaijenge Tanzania.